Utangulizi
Mkoa una jumla vituo 365 vinavyotoa huduma za Afya: Hospitali 13, Vituo vya Afya 50 na Zahanati 302
Kati ya vituo vya kutolea huduma 365, 198 (54.2%) vinamilikiwa na Serikali, 87 (23.8%) Binafsi, 69 (18.9%) Mashirika ya Dini, na 10 (2.7%) Mashirika ya Umma
Kati ya hospitali 13,Serikali inamiliki 4 (30.8%),mashirika ya dini 8 (61.5%),mashirika ya uma 1 (7.7%),binafsi 0
Lengo la Kitaifa ni kila halmashauri kuwa na hospitali ya halmashauri,kila Kata kuwa na Kituo cha Afya na kila Kijiji/Mtaa kuwa na Zahanati kwa asilimia
Maelezo
Ukilinganisha na robo iliyopita viwango vifuatavyo vimeongezeka:
Mahudhurio ya wajawazito kliniki toka 23.1% hadi 27%
Matumizi ya njia za uzazi wa mpango toka 40% hadi 40.8%
Upimaji wa watoto wachanga VVU toka 95% hadi 99.6%
Chanjo ya penta 3 toka 97 hadi 102%
Vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi Jan-Machi 2017
Halmashauri
|
Kituoni
|
Jamii
|
Jumla
|
Arusha Jiji
|
3
|
0
|
3
|
Arusha DC
|
0
|
0
|
0
|
Karatu
|
2
|
2
|
4
|
Longido
|
2
|
0
|
2
|
Meru
|
2
|
1
|
3
|
Monduli
|
1
|
0
|
1
|
Ngorongoro
|
0
|
1
|
1
|
JUMLA
|
10
|
4
|
14
|
Sababu zinazoongoza kwa vifo
Kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua-6(43%)
Embolism-3(21%)
Kupasuka kizazi(Ruptured uterus)-2(14%)
Mikakati iliyopo:
Halmashauri zimeshauriwa kufanya yafuatayo:
Kutumia fedha za uchangiaji kuomba oda maalum (Special Request) MSD kulingana na utaratibu waliotupatia
Kuweka kwenye bajeti maombi ya vibali vya ajira
Kutenga bajeti za ujenzi/ukarabati wa bohari za dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya
Ufuatiliaji wa matumizi ya dawa vifaa tiba na vitendanishi wakati wa ziara za usimamizi
Ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mt. Meru kuanza ujenzi wa Hospitali za Wilaya pamoja na ujenzi wa ukarabati wa Vituo vya Afya katika Mkoa wangu umeendelea kama ifuatayo:-
Awamu ya Kwanza kwa ujenzi na ukarabati wa vituo vya Afya na tulipata kiasi cha shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya Vituo 2.Kituo cha Afya Kambi ya Simba kilichopo Halmashauri ya Karatu wamepata Kiasi cha Tsh.Milioni 500, na Kituo cha Afya Nduruma kilichopo Arusha DC wamepata Kiasi cha Tshs.Milioni 500.Sambamba na fedha hizi kila kituo kimetengewa kiasi cha Tshs milioni 220 kwa ajili ya Vifaa.
Awamu ya Pili tulipata kiasi cha shilingi cha Bilioni 3.1 kwaajili ya ukarabati wa vituo vifuatavyo:-
Aidha,Hospital ya Rufaa ya Mt. Meru imepokea sh.1,145,000,000 kwa awamu ya kwanza kwa ajili ya ujenzi wa Wodi Grade I na ICU.
Jiji la Arusha limeanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwa Ujenzi wa jingo la wagonjwa wan je (OPD) ambalo lipo hatua ya kupaua ambapo Jiji limetenga sh.535, 518,225 kwa mapato ya ndani.
Pamoja na ukarabati huu kuendelea bado tunatarajia kuboresha Huduma ya afya katika;
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Sanduku la Barua: 3050 Arusha
Simu: 27 254 5608
Simu Nyingine: 027 254 4950
Barua Pepe: ras@arusha.go.tz
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa