• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

Ufugaji

Mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano, kwa mujibu wa ILANI ya Chama Cha Mapinduzi, katika kuindeleza sekta ya mifugo ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa mitamba, kupima na kumilikisha wafugaji maeneo ya ufugaji, kujenga miundombinu ya mifugo na kueneza uzalishaji wa mifugo bora. Katika kutekeleza azma hiyo ya Serikali Mkoa wa Arusha umetekeleza mikakati mbalimbali ya kuiwezesha sekta ya mifugo kutoa mchango stahiki kwenye kukuza uchumi wa nchi na kuongeza kipato, kama ifuatavyo:-

  • Usambazaji wa mitamba- jumla ya mitamba 4,067 imesambazwa kwa wafugaji kupitia mamlaka za serikali za mitaa zote katika Mkoa wa Arusha. Hii ni sawa na asilimia 22 ya lengo la Mkoa la kusambaza jumla ya mitamba 18,210 ifikapo mwaka 2020;
  • Umilikishaji wa maeneo ya ufugaji-
  • maeneo yenye ukubwa wa hekta 54,596 zimepimwa na kumilikishwa kwa wafugaji kwa ajili ya malisho ya mifugo;
  • jumla ya wafugaji wa asili 1,960 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuanzisha mashamba ya malisho;
  • jumla ya mashamba ya malisho 18 yameanzishwa kwa ajili ya wafugaji kuhifadhi malisho na kuyatumia wakati wa ukame.
  • Ujenzi wa miundombinu ya mifugo na masoko-
  • Jumla ya Majosho 9 yamekarabatiwa kati ya lengo la kukarabati majosho 33;
  • Visima virefu 7 vimechimbwa kwa ajili ya kunyweshea mifugo;
  • Jumla ya viwanda 3 vya nyama na mazao mengine ya mifugo vimeanzishwa katika Halmshauri ya Meru.
  • Mikopo kwa vikundi vya wafugaji-
  • Jumla ya vikundi 46 vya wafugaji vimewezeshwa na kupata mikopo katika taasisi kwa ajili ya ufugaji wa Ng’ombe, mbuzi, na wanyama wengine.
  • Jumla ya ng’ombe 242 walikopeshwa kwenye vikundi vya wafugaji kupitia utaratibu wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe umefanyika.
  • Programu za mafunzo ya ufugaji wa kisasa-
  • Jumla ya vikundi 84 vya wafugaji vimepatiwa mafunzo juu ya ufugaji bora na wa kisasa;
  • Jumla ya wafugaji 7,947 wamefundishwa mbinu ya ufugaji bora, umiliki wa ardhi na namna ya kupata mikopo.
  • Afya ya mifugo-
  • Jumla ya ng'ombe 469,481, mbuzi 533,482 na kondoo 9,832,600 wamechanjwa dhidi ya magonjwa ya Homa CBPP, RVF na PPR;
  • Jumla ya Dozi za magonjwa lita 528,710 zimesambazwa kwa ushirikiano na sekta binafsi kwa ajili ya chanjo na magonjwa ya mifugo.

 Sekta Ndogo ya Uvuvi

Kwa ujumla uendeshaji wa shughuli za uvuvi siyo eneo la kipaumbele sana kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha. Hii ni licha ya umuhimu iliyonayo sekta ya uvuvi katika kuimarisha lishe na kuongeza kipato cha wananchi. Kutokana na hali hiyo Serikali imekuwa ikiwahamasisha wananchi ili waweze kujihusisha na ufugaji wa kisasa wa samaki kwa kutumia mabwawa madogo. Ili kuweza kufikia azma hiyo shughuli kadhaa za uvuvi zimetekelezwa kwa uratibu wa Serikali ya Mkoa, kama ifuatavyo:

  • Jumla ya vikundi 19 vya wafugaji wa Samaki vimeanzishwa pamoja na kutoa mafunzo kwa wafugaji wa Samaki 416 kuhusu mbinu za uvuvi na ufugaji wa kisasa wa Samaki.
  • Jumla ya mabwawa 47 ya kufugia samaki yamejengwa  katika Jiji la Arusha na katika Halmashauri za Wilaya Karatu, Arusha na Meru;
  • Jumla ya wavuvi wadogo 233 wamehamasishwa kuchimba mabwawa madogo ya kuvulia sehemu maeneo ya ukame.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO KIDATO CHA NNE,KIDATO CHA PILI NA DARASA LA NNE. January 15, 2021
  • KERO ZA WANANCHI KUSIKILIZWA KILA SIKU July 14, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • ONGEZENI UFAULU WA SHULE ZA MSINGI-RC KIMANTA

    April 19, 2021
  • WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUPATIWA VYETI VYA KUZALIWA BURE

    April 16, 2021
  • JAJI MKUU-YAFAHAMUNI MABORESHO YA MAHAKAMA

    April 15, 2021
  • ZIARA YA WAZIRI WA ULINZI FALME ZA KIARABU

    April 08, 2021
  • Angalia Zote

Video

JIUNGENI NA BIMA YA AFYA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Sanduku la Barua: 3050 Arusha

    Simu: 27 254 5608

    Simu Nyingine: 027 254 4950

    Barua Pepe: ras@arusha.go.tz

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa